Pages

Sunday, August 5, 2012

HUYU MTU ANA MATATIZO GANI?

Habari zenu wakuu, nina mtu wangu wa karibu hali yake inanipa utata. Yeye yuko late 30's amelelewa kilokole na pia hivyo nyumbani kulikuwa na maadili mazuri yaani it was very strict family, mambo ya ujana kwao yalikuwa hayana sehemu, kwahiyo mambo ya watoto wa mjini kwake yalikuwa hakuna.


Sasa yeye ni mtu mzima, mamake na nduguze wamepiga dau la kuoa wamechoka maana kihali na mali inamruhusu (anaishi peke yake). Kitu cha kushangaza huyu mtu hajawahi kuwa wala kuonekana na GF kama kawaida ya wanaume. Hana hata mtoto wa kusingiziwa, yaani urafiki na wanawake hana hata ule wa platonic hakuna zaidi ya sisi jamaa zake. Nimejaribu kumconnect na sister fulani hivi poa, kwa kuhisi labda atakuwa domo zege nalo halikufaa maana ni muda wako pamoja lakini mazungumzo hayaendi next level.

Kuwa ni mlokole si mlokole...jamani kuna jinsia gani zaidi kwa mwanaume kama mtu si gay or straight kuna 3rd option?

No comments:

Post a Comment